Tarehe 6 Agosti, Mheshimiwa @anthony_mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe, alitembelea banda la SAGCOT Square katika maonesho ya NANE NANE MBEYA na kushuhudia Kliniki ya Kilimo Biashara iliyoendeshwa na @360connecttz chini ya mradi wa FEED THE FUTURE TANZANIA – Kilimo Tija (Horticulture Productivity Project). Kliniki hiyo ilijumuisha AMCOS, SMEs, na wajasiriamali, na ililenga kutoa huduma zifuatazo:
-Elimu kuhusu Kodi na wajibu wa Mlipa Kodi
-Mchakato wa kupata vibali vya TBS na SIDO
-Mafunzo kutoka kwa Afisa Biashara
-Mbinu za Kukuza Masoko Kidigitali.
Mhe. ANTHONY alisisitiza Wakulima wauze kutokana na uzalishaji na sio kwa bei ya hasara kwa maendeleo mazuri ya uzalishaji. Pia Alitoa wito kwa Wadau mbalimbali wa Fedha kama Banks ( CRDB ) wajikite kutoa fursa walizonazo kuhusu kilimo ( Mazao ) katika kuwezesha vitendea kazi kwa Manufaa ya maendeleo ya Nchi. Kwa kutambua hilo 360 Connect linajikita katika kusaidia wakulika katika uhusiano wa masoko ( Market Linkage ) kuhakikisha mkulima anapata soko husika kabla hajatoa Mazao Shambani.
Kliniki hii ilihuzuliwa na wabobezi mbalimbali kutoka TRA, SIDO, TIGO, LEOLEO APP, TBS na Afisa Biashara wa Jiji.